Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amesema kuanzia sasa uhamisho wa watumishi wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa utafanyika mara nne kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Shemdoe amesema kila tarehe 10 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka uhamisho utafanyika na majina yatawekwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

“Robo kwanza ya mwaka kuanzia Julai – Septemba majina ya uhamisho yatakua yatatoka tarehe 10 October , na robo ya Pili Oktoba – Desemba majina ya uhamisho yatatoka Januari 10.” amesema Shemdoe na kuongeza
kuwa: ” katika robo ya tatu ya Januari- Machi majina ya uhamisho yatatoka April 10 na robo ya mwisho ya Aprili-Juni majina ya uhamisho yatatoka Julai 10.”

Prof.Shemdoe amebainisha kuwa majina ya watumishi wote watakaopata uhamisho yatawekwa kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.

Sambamba na maelekezo hayo, Prof. Shemdoe amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuwasilisha orodha ya majina ya watumishi waliomba kuhama kuwasilishwa majina hayo ofisi ya Rais-TAMISEMI kila tarehe 05 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka.

Aidha, amewataka Makatibu Tawala wote kutokupitisha maombi ya watumishi wanaotaka kuhamia kwenye majiji, manispaa na miji kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya watumishi.

Aidha, Profesa Shemdoe aliwataka Makatibu Tawala kuwapa kipaumbele watumishi wenye changamoto mbalimbali zilizothibitishwa na Mamlaka husika ikiwepo Ugonjwa.

Prof. Shemdoe amewataka watumishi wote kubakia kwenye vituo vyao na barua za uhamisho zitatumwa kwa waajiri lakini pia wataona majina hayo kupitia Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI

Prof. Shemdoe ametoa uangalizi kwa watumishi dhidi ya matapeli wanaotaka fedha kwa ajili ya kufanikisha uhamisho, suala la Uhamisho ni bure na ni haki ya kila Mtumishi hivyo epukeni matapeli.

Kuhusu barua za Uhamisho za kipindi cha nyuma ambazo zilishafika Ofisi ya Rais TAMISEMI, zinashughulikiwa na majina yatatolewa kila mwezi mpaka Juni 30 kabla utaratibu mpya haujaanza kutumika.

Polisi yapiga mkwara mashabiki Simba, Yanga
KMC FC waifuata Namungo FC