Katibu Mkuu OR- TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza uongozi wa Jiji la Dar es salaam kuanza kuwalipa walimu wa shule za msingi 102 waliostaafu kuanzia mwaka 2018 ambao wanadai fedha za mizigo.

Prof. Shemdoe ametoa agizo hilo wakati akizungumza na walimu hao Jijini Dar es Salaam ambapo amesema wataanza kulipwa kuanzia wiki ijayo.

‘‘Suala la kusafirisha mizigo baada ya kustaafu kwa walimu 102 waliostaafu Aprili – Disemba ,2018 malipo yao yameshahakikiwa wanadai na Jiji la Dar es Salaam na watalipwa kuanzia wiki ijayo na fedha zilizolipwa ni takribani sh. Mil 210.

Prof.Shemdoe amesema kuwa watumishi wengine 102 walioistaafu kati ya Januari – Disemba 2019 na 14 waliostaafu mwaka 2021 wenye jumla ya madai ya sh. Mil 368 amemuelekeza Mkurugenzi wa Jiji hilo kufanya ‘realocation’ kwenye Bajeti yake mwezi Dec ili aweze kuwalipa ifikapo februali 2022.

Aidha, Prof. Shemdoe amewaelekeza Uongozi wa Jiji kujiridhisha tena kama kweli wengi wao hawastahili kulipwa kwa kuwa walikua wanahamishiwa vituo vya kazi ambavyo havikuwagharamu kuhamisha makazi.

Kikao hicho ni utekelezaji wa Agiza la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI alilolitoa mnamo Tar . 28.10.2021 wakati waaataafu hao walipokuja Ofisini kwake kuwasilisha changamoto zao.

Wanaharakati waitisha maandamano Sudani
Rais Samia atuma salamu za pole kwa Jaji Mkuu