Mbunge wa Jimbo la Mikumi kwa tiketi ya Chadema, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amefunguliwa Kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wake.

Kesi hiyo ya Uchaguzi imefunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jonas Nkya.

Nkya aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni kuwa amefungua Kesi hiyo akiiomba mahakama kubatilisha ushindi wa Profesa Jay kutokana na utata uliojitokeza wakati wa kutangaza matokeo.

“Uchaguzi huu utarudiwa, nadhani wote mliona utata uliojitokeza wakati wa kutangaza matokeo ya Jimbo la Mikumi, “Nkya alisema.

Mpango wa Ukawa Kuunda Chama Kimoja Cha Siasa Huu Hapa
Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza, Afunguka