Msanii mkongwe wa muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametangazwa rasmi kuwa mbunge mpya wa jimbo la Mikumi kwa tiketi ya Chadema baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu wa CCM, Jonas Nkya.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na msimamizi uchaguzi, Profesa Jay ameshinda kwa kura 32,256, kura ambazo zimempa ushindi wa tofauti ya kura 1834 kwani mpinzani wake huyo amepata kura 30425.

Hata hivyo, CCM imefunika zaidi katika viti vya udiwani baada ya kuchukua kata 11 huku Chadema wakipata kata 4. Hivyo, CCM itaongoza Halmashauri hiyo yenye kata 15. Hivyo, Profesa Jay atakuwa na changamoto katika baadhi ya maamuzi ya halmashauri.

Profesa Jay Chadema

Profesa Jay sasa ataungana Bungeni rapa mwenzake mkongwe ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Jimbo la Kilosa Kati pia limechukuliwa rasmi na Chama Cha Mapinduzi CCM. CCM pia wameshinda katika jimbo la Mvomelo, baada ya mgombea wake Nurad Sadick kupata kura 67,190 akimpita mshindani wake Mchungaji Oswald Mlai wa Chadema aliyepata kura 32,797.

CCM Na Chadema Waibuka Tena Majimbo Mkoa Wa Mara
Ligi Kuu Ya Vodacom Kuendelea Kesho