Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amempa mkono wa heri na kwaheri Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura aliyemaliza muda wake wa ubalozi nchini.
Prof. Kabudi amempongeza Balozi huyo wa Rwanda kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania. Waziri huyo alitoa pongezi hizo katika hafla fupi iliyofanyika jana, Septemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam.
Alieleza kuwa nchi hizo zitaendelea kushirikiana kwa karibu zaidi katika maeneo mawili muhimu ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika kusambaza madawa maeneo ya vijijini na Teknlojia ya Habari na Mawasiliano.
Naye Balozi Kayihura ambaye amefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano nchini, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.
Alielezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na alipongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo.
Akizunumzia mafanikio yaliyojitokeza kutokana na ushirikiano huo, Balozi Kayihura alisema hatua zinazochukuliwa zimefanikisha kuongeza idadi ya wafanyabiashara wa Rwanda kutumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizogo hadi kufika asilimia 98