Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amewataka wanananchi kumuamini katika nafasi yake hiyo mpya kwani ndiye sehemu ya taaluma yake.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Maghembe ameeleza kuwa kwa kuwa ‘uprofesa’ wake unatokana na Maliasili na Utalii atafanya kazi yenye mafanikio.

Profesa Maghembe aliwatangazia watu wanaohujumu maliasili kwa kufanya ujangili kuwa kiama chao kimefika.

“Hawa ambao wanaiba, wanajangili, wale ambao wanakata magogo na kuyasafirisha nje… kiamo chao kimefika,” alisema Profesa Maghembe ambaye uteuzi wake umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii na wachambuzi wa masuala ya kisiasa.

Wamiliki wa Hotel Zilizoko Ufukweni Wapigwa Marufuku Hii
Mvutano kati ya Mr. Blue na Diamond kuhusu Jina 'Simba' wazua Gumzo