Uwepo wa Programu ya Kuendelea Sekta ya kilimo na Uvuvu – AFDP, itasaidia kuiwezesha jamii kupewa elimu ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya kisasa, huku ikiwajengea uwezo vijana kupitia mafunzo kwa vitendo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga ameyasema hayo wakati wa ziara ya kufuatilia shughuli za utekelezaji wa Program hiyo, ambapo alitembelea katika Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira, Mkoani Morogoro.
Amesema, Ofisi yake inajukumu kubwa na kuratibu program hiyo itakayotoa fursa kwa kundi la Vijana kupata ujuzi kupitia mafunzo kwa vitendo yanayotolewa na kituo hicho huku akiwaasa kuzingatia elimu wanayopata na kujali muda wanaoutumia ili kuwa na matokeo tarajiwa.
.Awali, akitoa taarifa ya utekelezaji wa program ya AFDP katika kituo, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira, Gilness Frank amiepongeza Serikali kwa kuendelea kuratibu uwepo wa program hiyo inayofadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo – IFAD.