Mshambuliaji mpya wa PSG, Lionel Messi anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wili mbili baada ya vipimo vya MRI kuonesha kuwa amepata mikwaruzi ndani ya goti lake la kushoto ambalo lilimfanya aanze kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Lyon mwishoni mwa juma lililopita..
Kwenye mchezo huo, Kocha wa PSG, Mauricio Pochettino aliishuku afya ya nyota huyo na kuamua kumfanyia mabadiliko dakika ya 75 na nafasi yake ilichukuliwa na mlinzi wa kulia, Achraf Hakini kwenye mchezo ambao ulizua gumzo baada ya Messi kufanyiwamabadiliko.
Messi tayari ameukosa mchezo mmoja wa Ligi kuu ya Ufaransa dhidi ya Metz usiku wa kuamkia leo Septemba 23, kwa PSG kupata ushindi wa mabao 2-1 na kufikisha alama 21 kwenye michezo yake 7 na kuwa na ushindi wa asilimia mia moja.
Maumivu ya goti yanayomkumba Messi na kutazamiwa kumuweka nje kwa wiki mbili, yatamfanya akose mchezo wa Liguue w dhidi ya Montepelier na hata ule wa Manchester City kwenye Ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa Septemba 28 mwaka huu.
Wakati Lionel Messi anaumia, kiungo Maeco Verratti na Mlinzi wa kati Sergio Ramos wameanza mazoezi ya kujiweka fiti zaidi ili ajitupe dimbani.