Rais wa Klabu bingwa nchini Italia SSC Napoli, Aurelio de Laurentiis amefunguka hadi sasa timu pekee ambayo inaweza kumsajili mshambuliaji wao Victor Osimhen, ni Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain na imeonyesha nia ya kutoa Euro 150 milioni kama ada ya usajili.

Osimhen mwenye umri wa miaka 24, huduma yake inahitajika na vigogo wengi barani Ulaya, kwa sasa anaangaliwa na mabosi wa PSG kama mbadala wa Kylian Mbappe.

Licha ya utitiri wa timu hizo nyingi zinazohitaji huduma fundi huyu, shida kubwa imeku wa ni kiasi cha pesa ambacho SSC Napoli inakihitaji na timu nyingi zinaonekana kushindwa.

Licha ya Aurelio kudai PSG pekee ndio inaweza kumnunua Osimhen, timu hii itaweza kutoa pesa ya kumnunua Mshambuliaji huyu wa kimataifa wa Nigeria ikiwa tu itamuuza Mbappe.

Mkataba wa sasa Osimhen mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Msimu uliopita alicheza mechi 39 za michuano yote na kufunga mabao 31.

Msiwafiche watoto wenye ulemavu timizeni ndoto zao - DC Sima
Raila rafiki wa Wajackoya 'mabangi' unatarajia nini - DP Gachagua