Klabu ya Paris Saint-Germain inafikiria kuvunja mkataba na beki wao kutoka nchini Hispania Sergio Ramos, waliyemsajili miezi michache iliyopita akitokea Real Madrid.
Taarifa za pande hizo mbili kutarajia kuachana, zimeanikwa hadharani, Jarida la Les Parisien.
Ramos mwenye umri wa miaka 35, alisajiliwa kama mchezaji huru katika majira ya joto, lakini hajafanikiwa kucheza mchezo wowote akiwa na PSG kutokana na majeraha yanayomuandama hadi sasa.
PSG wanadai hawakupewa taarifa sahihi na za kutosha kuhusu majeraha ya mchezaji huyo wakati wa usajili wake na wako tayari kuvunja mkataba ili wapunguze gharama za mshahara.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, PSG inaweza kuachana na mchezaji huyo wakati wowote kuanza sasa na atakuwa huru kujiunga na timu yoyote.