Wachezaji wa Paris St Germain na familia zao jana walipata wakati mgumu walipowasili jijini Paris nchini Ufaransa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bourget, kufuatia karaha walizozipta kutoka kwa mashabiki ambao walichukizwa na matokeo ya kufungwa mabao sita kwa moja dhidi ya FC Barcelona.

Mashabiki hao wameripotiwa kuwafanyia vurugu wachezaji kwa kuwarushia maneno mazito mazito na wengine walidiriki kuambiwa wameihujumu PSG kwa manufaa yao binafsi.

Uongozi wa klabu hiyo inayoshikilia taji la Ufaransa, umetoa taarifa hizo kupitia tovuti ya PSG na kuonyesha masikitiko ya tukio hilo, ambalo halikubeba uungwana kwa wachezaji na familia zao.

Uongozi wa PSG pia umetumia nafasi hiyo kuwataka radhi mashabiki wote, kutokana na matokeo waliyoyapata katika mchezo wa mkondo wa pili wa 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona.

PSG walikua wanaongoza mabao manne kwa sifuri kabla ya mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa usiku wa kuamkia jana, na walipaswa kuulinda ushindi huo, lakini hali ilikua tofauti na kujikuta wakiangushiwa kipigo cha paka mwizi.

Mashabiki wengi wa PSG waliamini mambo yangekua mazuri upande wao na kuiona timu yao ikisonga kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, na badala yake walijikuta wakipandwa na hasira kwa matokeo tofauti.

Pep Guardiola Kumvuta Dani Alves
Bacary Sagna Kurudi Jijini London