Klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) imetoa tamko la kumuunga mkono mshambuliaji Neymar da Silva Santos Júnior, kufuatia tukio la kibaguzi analodaiwa kufanyiwa, wakati wa mchezo wa Ligi mwishoni mwa juma lililopita.

Mchezo huo ulioshuhudia Paris Saint Germain wakipepetana dhidi ya Olympic Marseille, uligubikwa na vurugu dakika mbili kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa na mwamuzi, huku chanzo kikitajwa ni rafu aliyochezewa mchezaji wa Marseille, iliyochagizwa na maneno ya kibaguzi kwa wachezaji wa timu pinzani.

Tukio hilo lilizua songombingo kubwa na kupelekea mwamuzi kutumia usaidizi wa VAR, na baadae kutoa adhabu ya kadi tano nyekundu.

Taarifa iliyotolewa na PSG kupitia kurasa za mitandao ya kijamii imeeleza kuwa: “Hakuna nafasi ya ubaguzi kwenye jamii, soka au maisha yetu. Tunategemea kamati ya maadili kupitia LFP itafanya uchunguzi wa kina na kutoa majibu sahihi. Klabu ipo tayari kushirikiana na LFP kama itahitajika.”

Membe kuanza kampeni rasmi Tabora
TANESCO: Msiunganishe umeme kiholela, Tuwe wazalendo