Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain usiku wa kuamkia leo walikamilisha usajili wa kiungo kutoka nchini Brazil Rafael Alcântara do Nascimento (Rafinha), akitokea FC Barcelona.

Kiungo huyo ambaye ni ndugu wa damu wa Thiago Alcantara, amejiunga na miamba hiyo ya jijini Paris akiwa mchezaji huru, baada ya kuenguliwa kwenye mipango ya meneja mpya wa FC Barcelona, Ronald Koeman.

Licha ya kuondoka kama mchezaji huru, Paris Saint-Germain wameingia makubaliano maalum ya kuilipa FC Barcelona asilimi 35 ya fedha zitakazopatikana, endapo watamuuza kiungo huyo kwenye klabu yoyote kwa siku za usoni.

Hata hivyo Rafinha anaondoka FC Barcelona baada ya kutolewa kwa mkopo kwa nyakati tofauti kwenye klabu za Celta Vigo msimu wa 2019/20, na kabla ya hapo alicheza kwa mkopo Inter Milan msimu wa 2018/19.

Rafinha ambaye ni mzaliwa na Brazil, alikulizwa kwenye kituo cha kulea vijana kisoka cha FC Barcelona (La Masia,) na alicheza michezo 90 akiwa na kikosi cha kwanza cha klabu hiyo baada ya kupandishwa mwaka 2011.

Alicheza kikosi cha kwanza cha FC Barceona kuanzia mwaka 2011 hadi 2013.

Anakuwa mchezaji watatu kusajiliwa na Paris Saint-Germain katika siku ya mwisho ya dirisha la Usajili kufuatia kuwasili kwa Moise Kean kwa mkopo akitokea Everton na Danilo Pereira kwa mkopo kutoka FC Porto.

Lil Ommy, DJ Sinyorita watajwa Marekani, kuwania Tuzo, Diamond afunika
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 6, 2020