Klabu ya Paris St-Germain ikicheza bila mshambuliaji wake Neymar Jr imeshindwa kupata pointi tatu katika ligi kuu ya Ufaransa ‘League 1’ kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kupata sare ya 0-0 na klabu ya Montpelleir.

Neymar ambaye hivi karibuni alitofautiana na Edinson Cavani kuhusu ni nani angepiga penati katika mechi yao ya mwisho dhidi Lyon, anasumbuliwa na jeraha dogo la mguu.

Wakati PSG wakiambulia sare katika mchezo huo, Monaco ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa wameibuka na Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya klabu ya Lille.

Mabao ya Monaco yalifungwa na Radamel Falcao aliyefunga mabao mawili na kutimiza mabao 11 katika michezo saba ya League 1 aliyocheza huku mabao mengine yakifungwa na Stevan Jovetic pamoja na Rachid Ghezzal.

Kwa sasa Paris St-Germain wako kileleni mwa League 1 wakiongoza kwa pinti 19 huku Monaco ikiwa katika nafasi ya pili kwa kukusnya pointi 18 katika michezo 7 iliyokwisha cheza mpaka sasa.

 

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 25, 2017
Lebron James amtusi Trump