Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umefanya malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 880 kwa wastaafu elfu 10,000 ambao walikuwa wanadai malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi.

Hayo yamesemwa na Meneja Kiongozi wa Mfuko huo, Eunice Chiume ambapo amesema kuwa malipo hayo yamefanyika katika kipindi cha mpito kilichotolewa na Serikali kuanzia  Agosti 2018 hadi Februari 2019.

amesema kuwa hatua hiyo ni mwaka mmoja, tangu mfuko huo uanze kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 baada ya Serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

“Ili kuhakikisha PSSSF inatoa huduma bora na za haraka, imefungua ofisi mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na tunatoa wito sasa, kwa wale wastaafu takribani elfu 10,500 ambao bado taarifa zao hazijahakikiwa wafike kwenye ofisi zilizo karibu nao ili kukamilisha zoezi hilo muhimu linalofanyika kila mwaka.”amesema Chiume

Aidha, kuhusiana na suala la uhakiki, Chiume amesema kuwa Lengo la uhakiki ni kuupa Mfuko fursa ya kufanya malipo kwa usahihi na kwa mtu anayepaswa kulipwa kwani taarifa zinaweza kubadilika ikiwa ni pamoja na zile za kibenki huenda mhusika akahama kutoka benki moja kwenda nyingine, mabadiliko ya wategemezi lakini hata kifo pia.

Zao la Muhogo lakosa soko, Wakulima waiangukia Serikali, 'Tusaidieni jamani'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 15, 2019