Shule Kongwe ya Wavulana ya Pugu Sekondari iliyopo Manispaa ya Ilala Gongo la Mboto iliyotoa viongozi wakubwa wa Nchi hii akiwemo Hayati, Mwalimu Julias Kambalage Nyerere na viongozi wengine wakubwa imekuja mikakati ya kuendeleza utoaji wa wanafunzi watakao kuwa viongozi wakubwa wa Nchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Shule hiyo, Juma Boneface Orenda wakati akizungumza na mwandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kutoa huduma bora katika sekta ya elimu.

Amesema, “Sekondari yetu ina watoto wapatao 930 kati ya hao 117 ni wenye mahitaji maalum, lakini tunamshukuru Dkt. Rais wetu kwani hata wanafunzi hao wenye mahitaji wanafanya vizuri sana madarasani lakini pia ninamuhakikishia Dkt. Samia kwamba walimu na watumishi wengine wasiokuwa walimu shuleni hapa katika kumuunga mkono Rais wanafanya kazi mzuri sana,” amesema Orenda.

“Shule hii ni kongwe sana na ilianza mwaka 1948 na sasa ina miaka 75 hivyo lazima tufanye kazi kwa bidii sana katika kuhakikisha historia ya kutoa viongozi wakubwa kwenye shule yetu inaendelea na huu ndio mkakati wetu tunaomba Mungu atusaidie,” alisema Mkuu huyo.

Amesema katika kuendeleza utaratibu wa kutoa viongozi wakubwa Sekondali ya Pugu amekuja na mfumo Mpya yaani Kifurushi cha maandalizi ya asubuhi kinachojulikana kama (Morning Preparation Package) inayosimamiwa na Mkuu wa Shule pamoja na Mwalimu wa siku hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa, tayari ameunda timu maalum ya taaluma shuleni hapo ambapo timu hiyo inafanya ziara katika mashule mbalimbali yanayofanya vizuri ili waweze kujifunza na kwamba tayari wamefanya ziara Tabora Boys pamoja na Bright Future Girls na baada ya hapo wanampango wa kutembelea shule ya Ilboru Boys iliyopo Jijini Arusha lengo likiwa ni kujifunza wanavyofanya vizuri Kitaaluma.

Mmoja wa Walimu wa Shule hiyo, Sala Mlangi naye amesema, “tunaendelea kumpa heko kwa kutupatia Vishkwambi (laptop) ambazo kwa namna moja ama nyingine zimeturahisishia kwenye utendaji kazi wetu na hasa nyakati za mitihani kwani kwa sasa hakuna haja ya kuandika kwenye makaratasi kama awali.”

Naye, Mwalimu Consolata Blasi, alisema pia mbali na hayo yote Rais Dkt. Suluhu, ameweza kuwapatia vitabu vya mitaala yote hivyo kuwafanya waweze kufanya kazi yao kwa uraisi tofauti na hapo awali.”

Hitimana: Nilijua kuna siku ningeondoka KMC FC
Manchester United hali tete Ulaya