Baadhi ya wafugaji wa Punda nchini Kenya, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wamefanya maandamano ya amani kupinga kufunguliwa tena kwa machinjio ya mnyama huyo, huku wakiitaka Serikali kutoruhusu jambo hilo.
“Tumekataa uchinjaji wa punda (Hatutaki kuchinja punda).” Walikuwa wakiimba wamiliki hao tukio ambalo linakuja mwaka mmoja baada ya Serikali kusitisha uchinjaji wa punda kwa ajili ya nyama na bidhaa nyinginezo.
Mwaka 2022, baadhi ya Wanaharakati wafungua mashitaka Mahakamani ili kusitisha biashara ya nyama ya punda nchini humo ambayo ilikuwa ikiuzwa nje ya Kenya.
Kupitia kesi hiyo, Wanaharakati hao, walibainisha kuwa wanyama hao hutumika kwa matumizi mengine ikiwemo Kilimo na ubebaji mizigo na sio nyama na kupelekea Mahakama kutoa amri iliyokataza kuchinja Punda.