Chelsea watajaribu kuwazidi kete Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Pedro, 28 (Mail)

Chelsea watafikiria kuongeza dau na kufikia pauni milioni 40 kumsajili beki wa Everton John Stones, 21, baada ya dau la pauni milioni 30 kukataliwa (Guardian)

Fernabahce watamshawishi beki wa Chelsea John Terry na mshahara wa pauni milioni 2.5 kwa mwaka ili ahamia Uturuki (Mail)

Branislav Ivanovic, 31, huenda akawekwa bench na Jose Mourinho baada ya Chelsea kumsajili Abdul Baba Rahman ambaye anaweza kuanza siku ya jumapili dhidi ya West Brom (Mirror)

Manchester City watakamilisha usajili wa pauni milioni 88 kwa beki wa Valencia Nicolas Otamendi na Kevin De Bryce (Mirror)

West Brom wamewaambia Tottenham kuwa watahitaji kutoa pauni milioni 25 kumsajili Saido Berahino, 22 (Independent)

Bournemouth wanataka kumsajili mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe, 32, ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo akiwa bado kijana (Mirror)

Arsenal watahitaji kulipa pauni milioni 35 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani (Eurosport)

Real Madrid wana matumaini kuwa wanaweza kumtumia kipa Keylor Navas, 28, katika jitihada zao za kutaka kumsajili kipa wa Manchester United David De Gea, 24 (Marca)

Rais wa AC Milan Silvio Berlusconi amemwambia mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic, 33, kuwa anasubiriwa kwa “moyo mkunjufu” kurejea San Siro (Gazzetta World).

Chelsea Waipiku Man Utd Kumnasa Pedro
Berahino Apigwa Stop Kujiunga Na Spurs