Rais wa Russia Vladmir Putin siku ya ametoa nafaka ya bure kwa nchi sita za Afrika alipokuwa akizindua mkutano wake na viongozi wa bara hilo siku chache baada ya kujiondoa kwenye mkataba wa mauzo ya nafaka wa Ukraine.
Mkutano huo wa siku mbili wa Saint Petersburg alikozaliwa Putin unachunguzwa kama kipimo cha uungwaji mkono wake barani Afrika, ambapo anaendelea kuungwa mkono licha ya kutengwa kimataifa kulikosababishwa na uvamizi wake wa kijeshi wa kuivamia Ukraine mwaka 2022.
Mapema wiki iliyopita, Russia ilikataa kuongeza mkataba ambao ulihusika na mauzo ya nafaka ya Ukraine kupitia Black Sea kufika masoko ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Afrika na kupunguza shinikizo la bei ya vyakula.
Kupitia hotuba yake kwenye mkutano huo, Putin alisema Russia inaweza kutafuta mbadala wa nafaka ya Ukraine na kuahidi kupeleka nafaka katika nchi sita za Afrika.