Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesimamia luteka ya vikosi vya kimkakati vya nyuklia vya nchi hiyo, vilivyohusisha urushaji wa makombora ya masafa mafupi kwa kutumia meli za kivita.
Hayo, yamebainishwa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu na kusema luteka hizo ni majaribio ya mashambulizi makubwa ya nyuklia, ambayo watayafanya ili kulipiza kisasi, iwapo kutatokea shambulio la nyuklia dhidi yake.
Luteka hizo, zinatokea wakati kukiwa na mvutano mkubwa kati ya Urusi na Mataifa ya Magharibi kuhusu uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ametoa wito kwa wanasiasa kuachana na vitisho vya matumizi ya silaha za nyuklia katika vita vya Ukraine, na badala yake watafute suluhu ya kudumu ya amani.