Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya jamii ya kimataifa dhidi ya kuendelea kuiwekea vikwazo nchi yake kwa msingi ya uvamizi wao nchini Ukraine.

Akizungumza katika mkutano uliorushwa na kituo cha habari cha serikali Rossiya 24, Putin alionya dhidi ya mataifa yanaoyopinga uvamizi wao nchini Ukraine kuendelea kuikwanza Urusi na kuongeza kuwa Urusi haina nia mbaya katika ardhi ya jirani ila ameonya kuwa kuwekwa kwa vikwazo zaidi huenda kukachochea mahusiano mabaya zaidi kati ya Urusi na Ukraine.

“Hatuna nia mbaya dhidi ya majirani zetu. Nadhani kila mtu lazima afikirie jinsi ya kurekebisha uhusiano, kushirikiana kawaida na kukuza uhusiano kama kawaida,” Putin amenukuliwa.

Usemi wa Rais Putin umejiri huku mawaziri wa masuala ya kigeni wa mataifa ya Magharibi wakitua katika jiji kuu la Ubelgiji, Brussels, kujikuna vichwa jinsi ya kuhakikisha kuwa Urusi inakomesha uvamizi wake nchini Ukraine.

Juzi, Putin alimwambia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuwa nchi yake itatimiza malengo yake kwa Ukraine bila kujali chochote kitakachotokea.

Kupitia kwa taarifa baada ya marais hao wawili kuzungumza kwa njia ya simu, Kremlin iliweka wazi malengo ya uvamizi wake yanayojumuisha kumaliza silaha hatari za Ukraine na taifa hilo pia kutoegemea upande wowote.

Young Africans yaahidi furaha Mwanza
Fiston Mayele: Naitaka tuzo ya mfungaji bora 2021/22