Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema opereshion yake ya kijeshi nchini Ukraine ilikuwa ni lazima ifanyike.
Amesema hayo katika hotuba yake kuhusu mgogoro wa Ukraine, Putin amesema operesheni hiyo ilikuwa ni chaguo pekee lililokuwa limesalia kumaliza umwagaji damu wa miaka mingi Mashariki mwa Ukraine.
Putin amesema Ukraine imekuwa ikiandaa mashambulizi makubwa yanayolenga kurejesha maeneo yaliyojitenga ya Donbass ambapo zaidi ya raia 14,000 wakiwemo watoto wameuawa.
Kwa mujibu wa Putin, Kiev imekuwa ikiratibu mpango wa kuishambulia Crimea ambayo ilijitenga na nchi hiyo mwaka 2014 na kujiunga na Urusi kwa kura ya maoni.
“Imekuwa ikitiwa moyo na Marekani pamoja na nchi za Magharibi, Ukraine ilikuwa ikijiandaa kwa makusudi na kutekeleza mauaji huko Donbass.
Shambulio kubwa la Donbass na baadaye Crimea lilikuwa suala la muda tu. Hata hivyo, Majeshi yetu yamesambaratisha mipango hii,” Putin alisema wakati wa hotuba yake.