Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Urusi, Vladmir Putin wamekutana katika mkutano wa pili wa siri ambao haukutajwa madhumuni yake ambao ulifanyika katika kikao cha kwanza cha mkutano wa mataifa ya G20.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika mara baada ya mkutano huo wa kwanza wa nchi zenye nguvu kiuchumi duniani G20, Ikulu ya White House haijataka kulizungumzia suala hilo, huku Trump akikana kufanyika kwa mazungumzo hayo.
Aidha, Uhusiano wa viongozi hao wawili unachunguzwa kufuatia madai kuwa Kampeni za Rais Trump katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani alisaidiwa na Urusi, huku Wapelelezi wa Marekani wakiamini kuwa Urusi ilimsaidia Trump kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kitu ambacho Urusi imekana kuhusika.
Hata hivyo, Rais wa Marekani katika mkutano huo uliochukua muda wa saa moja hakua na msaidizi wake huku Vladmir Putini akiongozana na mkalimani wake ambaye ndiye alikuwa kiungo katika mazungumzo hayo.