Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekanusha taarifa za uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika Kata ya Goba, Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam ambazo zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, huku ikiwatoa ikiwatoa hofu Wananchi kuwa imefuatilia na kujiridhisha kuwa tarifa hizo sio za kweli na kuitaka jamii kuipuuza.

Taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Emmanuel Nonga imesema tangu Oktoba 12, 2023 kumekuwa na picha ya mayai mengi na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika Kata ya Goba, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amesema picha hiyo imembatana na maneno, “Serikali Hailali Kama alivyo Shetani Halali!! Wanajua kabisa Kwa sababu Shetani Halali kwa hiyo Kuna Mambo Mabaya atayatenda tu!! Kiwanda Cha mayai Goba Kwa wachina kimekamatwa Sasa hayo Mayai Yote Sijui yametagwa na Kuku Gani? Tusubiri yanayojiri, Usikie Technologia ilivyo hapo Ndiyo utakapojua Kwa nini kila Mtu Ana Kitambi.”

Aidha, imesema taarifa hizo zimetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu tasnia ya kuku nchini inayokuwa kwa kasi ambapo katika kufuatilia zaidi, Wizara imebaini kuwa picha hiyo ya mayai mengi iliyotumiwa ilionekana kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2016 na haikupigwa hapa nchini.

“Kuna kipande cha video (video clip) ya kijana anauza mayai ya kuchemsha ambayo yana viini viwili ambapo baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wanasema mayai haya yanatengenezwa viwandani na yanaweza kuwa hatarishi kwa afya ya binadamu. Mayai yenye viini viwili hayatengenezwi viwandani bali yanatagwa na kuku kama kawaida,” amesema.

Hata hivyo, tarifa hiyo imetaja sababu zinazopelekea yai kuwa na viini viwili ni pamoja na Umri wa kuku, mara nyingi hutokea kwa kuku wanaoanza kutaga au wanaomalizia umri wa kutaga, Chakula wanachopewa chenye virutubisho vingi kuku huweza kuwa na mayai yenye viini viwili, Kuwasisimua kuku kwa mwanga na aina ya kuku.

Leroy Sane kurudi England Januari 2024
Alexander Arnold: Sina nafasi maalum uwanjani