Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Angela Kairuki, amemkabidhi Ngao ya Ushindi wa Kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge baada ya Mkoa wa Pwani kuibuka mshindi katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2022/23.

Makabidhiano ya ngao hiyo ya ushindi, yameshuhudiwa na Katibu Tawala Mkoa na Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Mchata ambao kwa pamoja walionesha kufurahi mafanikio ya ushindi huo wa nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2022/23.

Zifuatazo ni Picha za kumbukumbu wakati wa makabidhiano ya Ngao hiyo, iliyotolewa jijini Dodoma Agosti 29, 2023.

Waziri Kairuki, akikabidhi Ngao ya Ushindi wa Kwanza kwa RC. Kunenge (katikati), kulia ni Katibu Tawala Mkoa huo na Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Mchata.
Picha ya pamoja kufurahia Ngao ya ushindi utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2022/23.

JKT Queens kufuata nyayo za Simba?
Usiri wagubika mazishi ya Prigozhin, Putin ajiweka kando