Msemo wa kichaga ‘tusileteane undugu kwenye hela’ umepata mfano baada ya kaka yake mfalme wa RnB duniani, R Kelly kumshitaki mwimbaji huyo akidai pesa yake.

Kwa mujibu wa TMZ, kaka yake R. Kelly anaefahamika kwa jila la Bruce Kelly amemfungulia mashtaka mwimbaji huyo akidai kuwa alimfanyia kazi kwa muda wa saa 144 kama msaidizi wake na dereva wake kwa makubaliano ya maneno kuwa angemlipa kiasi cha $700,000, lakini mwimbaji huyo hakufanya hivyo.

Kwa mujibu wa nyaraka za mashtaka yaliyowasilishwa na Bruce Kelly kwenye bodi ya kazi, ameeleza kuwa wakati mwingine alilazima kumsubiri R.Kelly kwenye gari kwa zaidi ya saa 12 na hakupata usingizi wowote.

Amesema alijaribu mara kadhaa kumwambia kaka yake huyo kumlipa deni lake lakini alionekana kutojali. Bruce amesisitiza kuwa hawezi kuweka miguu yake kwenye kazi ya mtu yoyote Yule bila malipo hata kama ni kaka yake.

R. Kelly bado hajazumgumza chochote kuhusu tuhuma hizi zilizotoka kwenye level ya familia hadi mikononi mwa serikali ikisukumwa na harufu ya fedha.

Avril Ahamishia Taarifa Za Ujauzito Wake Kwa Ndugu Yake
Kada aelezea kuvuja kwa ‘Mkakati wa Kumuengua Lowasa’