Baada ya beki wa Arsenal, Jurrien Timber kuumia, mpango wa timu hiyo ni kupata saini ya Joao Cancelo wa Manchester City, umerudi upya.
Timber aliumia katika mchezo wa ufunguzi wa Premier League dhidi ya Nottingham Forest uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo anatarajiwa kukosekana kwa takribani mwezi mmoja.
Kutokana na hilo, Arsenal inafanya juhudi kuipata saini ya Cancelo, huku kukiwa na taarifa kwamba, inataka kumuuza Kieran Tierney endapo watapata ofa nzuri.
Arsenal ikiwa inamuwania Cancelo, imeelezwa kwamba, inaweza kupata upinzani kutoka kwa FC Barcelona ambayo imekuwa ikimuwania kwa muda mrefu.
Katika majira haya ya joto, Arsenal imefanikiwa kusajili wachezaji wanne ambao ni Timber, Kai Havertz, Declane Rice na David Raya, huku ikiwa nà mpango wa kuwauza Tierney na Folarin Balogun.