Klabu ya Inter Milan imeanza chokochoko za usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Chile na klabu ya Arsenal ya England Alexis Sanchez.

Alexis, bado hajakamilisha mpango wa makubaliano ya kusaini mkataba mpya, kufuatia mkataba wake wa sasa na klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London kusaliwa na muda wa miezi 18.

Viongozi wa Inter Milan wanaamini wakati huu ni mzuri kwao kuanzisha chokochoko za usajili wa mshambuliaji huyo, ambaye bado anatafakari mustakabali wake ndani ya klabu ya Arsenal.

Kiasi cha Euro milioni 50, kinatajwa kutengwa na viongozi wa klabu hiyo ya mjini Milan kwa ajili ya uhamisho wa Sanchez, ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye orodha ya wamiliki wa Inter Milan Suning Holdings Group Co.Ltd.

Hata hivyo huenda Inter Milan wakapata upinzani mkali wa kumsajili Sanchez, kutokana na klabu nyingine kama Chelsea, PSG na Atletico Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Sanchez alisajiliwa na Arsenal miaka mitatu iliyopita akitokea FC Barcelona kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 31.7, na tayari ameshaitumikia The Gunners katika michezo 89 na kufunga mabao 44.

Video: Mbowe akanusha tuhuma za kuhusika na madawa ya kulevya
Harry Redknapp: Hart Anapaswa Kwenda Liverpool Sio Arsenal