Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England, Chelsea, Radamel Falcao anatafuta namna ya kuendelea kusalia Stamford Bridge, katika kipindi kilichobaki kabla ya msimu huu kufikia kikomo mwezi May mwaka huu.

Falcao, amelazimika kusaka njia hiyo, kutokana na uongozi wa klabu yake ya AS Monaco kuweka wazi kutomuhitaji tena katika mipango yao, huku akisisitiza hali yake ya majeraha ndio chanzo cha kumuweka pembeni.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Colombia, alilazimika kuondoka kwa mkopo nchini Ufaransa mwanzoni mwa msimu wa 2014-15, baada ya kusajiliwa na Man Utd, lakini hakua na bahati ya kumshawishi meneja wa Man Utd, Louis Van Gaal na hatimae mwishoni mwa msimu huo aliachwa.

Katika hali ya mshangao mwanzoni mwa msimu huu, aliyekua meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, alitangaza kumsajili kwa mkopo huku akiamini huenda angeweza kuleta ushindani katika safu yake ya ushambuliaji, lakini bado hali imeendelea kuwa ile ile kama alivyokua Old Trafford.

Kinachomsumbua Falcao hadi kushindwa kuonyesha uwezo wake kama alivyokua amezoeleka miaka ya nyuma, ni majeraha ya mara kwa mara.

Embedded image permalink

Falcao mwenye umri wa miaka 29, hakuwahi kucheza kwenye kikosi cha Chelsea tangu mwezi Oktoba mwaka 2015, kufuatia majeraha ya paja ambayo yalimkabili.

Makamu wa rais wa klabu ya AS Monaco, Vadim Vasilyev ametangaza msimamo wa kumuondoa Falcao kwenye mipango yao, alipokua akihojiwa na gazeti la Daily Motion.

“Falcao kwa sasa ni majeruhi, na huenda ikamchukua muda wa majuma sita hadi manane kupona. Lakini baada ya hapo itamlazimu kusaka mahala pengine pa kucheza soka lake.

Falcao kwa sasa amerejea katika klabu ya AS Monaco nchini Ufaransa, kwa ajili ya kuatiwa matibabu.

Changamoto nyingine ambayo huenda ikawa kikwazo kwa Falacao kucheza ama kutimiza malengo yake ya kusalia Chelsea, ni ushindani uliopo kwenye kikosi cha Chelsea kwa sasa kati ya washambuliaji Diego Costa pamoja na Loic Remy ambao mara kadhaa wamekua wakicheza kwa pamoja ama kwa kupokezana.

Mkataba wa Falcao na klabu ya AS Monaco, unatarajiwa kufikia kikomo mwaka 2018.

AS Monaco walimsajili mshambuliaji huyo mwaka 2013, akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa paund million 52, lakini alicheza soka kwa msimu mmoja kwa mafanikio katika ligi ya nchini Ufaransa (Ligue 1), kabla ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimlazimu kufanyiwa upasuaji.

Kim Poulsen Yu Njiani Kurejea Katika Soka La Bongo
Man city Wafanya Usajili Wa Kushangaza