Kamati ya Maudhui ya utangazaji imetoa maamuzi yake juu ya Radio 5 ya Jijini Arusha na Radio Magic ya Jijini Dar es salaam kufuatia ukiukwaji wa kanuni za utangazaji.

Maamuzi hayo yametolewa mapema leo septemba 16, 2016 na Makamu Mwenyekiti wa Mamati ya Maudhui, Joseph Mapunda ambapo amesema kuwa kituo cha kurushia matangazo cha radio 5 kimevunja kanuni za maudhui kwa kumkashifu Rais Magufuli na Serikali na kuchochea, kuhamasisha uvunjivu wa Amani na kupambana na Polisi.

Kamati hiyo imezitaja kanuni zilizokiukwa na kutoa maamuzi ya kukitoza faini kituo hicho ya shilingi milioni 5, kufungiwa kwa miezi 3 na kitakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mapunda pia ametoa onyo kali kwa kituo cha radio cha Magic cha Jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kukitaka kuomba radhi kwa Rais Magufuli pamoja na wananchi kuanzia Septemba 17 hadi 19, 2016 kwenye taarifa ya habari ya saa 10 jioni na saa 3 usiku.

Mkuu wa Upelelezi Kinondoni ahukumiwa kunyongwa, Zombe na wengine wapenya
Dirk Kuyt: Kauli Ya Pogba Ilinishangaza