Wakala wa Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Rafael Leao, ametoa taarifa kuhusu mazungumzo ya mteja wake ya kuongeza mkataba na AC Milan, akithibitisha kwamba majadiliano ni marefu.

Imeripotiwa sana siku za hivi karibuni kwamba nyota huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23, amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na ‘Rossoneri’ hao wenye thamani ya takriban euro milioni saba kwa msimu, ambao unajumuisha kifungu cha kuruhusiwa kuondoka cha euro milioni 150.

Mustakabali wa Leao umekuwa gumzo kuu linaloizunguka Milan msimu huu na klabu itatamani sana kurasimisha mkataba wake mpya hivi karibuni, ikitaka kuepusha vitisho vyovyote vinavyoweza kutokea katika dirisha lijalo la majira ya joto.

Akizungumza na Foot kuhusu mkataba wa Leao na Milan, Ted Dimvula wakala wa Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amethibitisha kuwa kazi inaendelea kukamilisha mpango huo.

Dimvula amesema; “Ndio, tunajadiliana na Milan kuongeza mkataba wa Rafael.

Kama ilivyo kwa ripoti yoyote ya ukubwa huu, majadiliano ni marefu na kila undani ni muhimu. Tunapanga kukutana saa chache zijazo kuhusu suala hili na uongozi wa klabu.”

Kwa Rafael, Milan ni klabu ambayo ni muhimu na matarajio yake hayajabadilika tangu awasili hapa. Anataka kucheza chini ya kocha ambaye anajua jinsi ya kumwendeleza, na anataka kucheza Ligi ya Mabingwa,” amesema wakala huyo.

Leao, ambaye alikosa mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Inter kutokana na jeraha, amefunga mabao 13 na kutoa asisti 13 katika mechi 44 katika michuano yote msimu huu.

Mke wa Thiago Silva akata mzizi wa fitna
Fahamu Kuhusu Zombie Apocalypse ya Meridianbet