Mcheza tenesi namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal ameshinda taji la 16 la Grand Slam na taji la tatu katika michuano ya US  Open baada ya kumshinda Kelvin Anderson kwa seti 6-3,6-3 na 6-4.

Imekuwa rahisi kwa Nadal kushinda Grand Slam  bila kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kutokuwepo kwa wakali kama Novack Djokovick, Andy Murray na Rodger Federer.

Rafael Nadal ilikuwa wazi asingepata upinzani mkubwa kwani wachezaji wote walioko katika 20 bora ya viwango vya tenesi walikuwa tayari wametupwa nje ya michuano hiyo na Nadal alichuana na mchezaji anayeshika nafasi ya 28 katika viwango vya tenesi duniani.

Hii ni Grand Slam nyingine kwa Nadal baada ya kushinda Grand Slam mwaka 2013 na inatimiza idadi ya Grand Slam 16 kwa Nadal huku akishinda mbele ya mashabiki wanaompenda kama mwenyeji wa hapo mjini NewYork.

Nadal sasa anakuwa na US Open 3 na kuwa na Grand Slam 16 akimkaribia kinara wa Grand Slam Rodger Federer ambaye hadi sasa ameweka kabatini jumla ya Grand Slam 19.

Shaka amtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, Malecela
Baba yake Mbwana Samatta aja na kitabu chenye siri ya mwanae