Mchezaji namba moja kwa ubora katika mchezo wa tenesi Hispania Rafael Nadal amefanikiwa kufika katika hatua ya robo fainali ya michuano ya China Open baada ya kumshinda Karen Khachanov wa Urusi.

Nadal mwenye umri wa miaka 31 alitawala mchezo huo na kumfunika kabisa Khachanov anayeshika nafasi ya 42 kwa ubora duniani nakufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali.

Mchezaji huyo ambaye alishinda taji la tatu la US Open mwezi uliopita ameshinda kwa seti 6-3 6-3 na katika hatua inayofuata atakabiliana na mchezaji wa Marekani John Isner, aliyemchapa Leonardo Mayer wa Argentina kwa seti 6-0 6-3.

Michuano ya China Open ni michuano ya tenesi ilioanzishwa mwaka 1993 na michuano hupigwa jijini Beijing ikiwa inashirikisha upande wa wanume na upande wa wanawake.

 

 

Video: Familia ya Lissu yamjibu IGP Sirro, Kiama raia wa kigeni
Kane aipeleka Uingereza kombe la dunia