Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Ismail Aden Rage ameingilia kati sakata la Kiugo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’, huku akimtaka kumuweka mbali mama yeke mzazi na suala hilo.
Feisal amekwama kwa mara ya pili katika Shauri la kutaka kuvunja mkataba na Young Africans mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’, baada ya kuomba kupitiwa upya kwa hukumu iliyotangazwa na Kamati hiyo mapema mwaka huu.
Rage amesema kitendo cha Feisal kumuingiza mama yake mzaizi katika sakata hilo ni kama amemdhalilisha mzazi wake, baada ya kuzungumza na vyombo vya habari siku moja kabla ya shauri lake kusikilizwa kwa mara ya pili.
“Kwa akili za kawaida kama kweli Feisal kama inavyosemekana alikuwa anakula ugali na sukari, anaenda mazoezini na bodaboda amezipata wapi pesa zaidi ya Milioni 100 za kuweka kwenye akaunti ya Yanga?”
“Huyu kijana alipaswa kuendelea na mambo haya kama alivyofanya katika hatua za awali, sasa kitendo cha kumuingiza mama yake na kusema maneno haya yote, ni kama amemdhalilisha mazazi wake,”
Katika hatua nyingine Rage amemtaka Feisal kuwa makini na anachokifanya kama anahitajika popote pale basi akutane na uongozi wa Young Africans atapewa thamani yake na kuwapelekea wanaomuhitaji
“Katika kitu ambacho FIFA wanapiga vita ni THIRD PARTY ni sumu mbaya kwenye biashara ya mpira haswa uhamisho wa wachezaji.” amesema Rage