Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Ismael Aden Rage amesema mpango wa waziri wa habari sanaa na michezo kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka 10 hadi 7 ni jambo jema.

Rage ameyasema hayo mara baada ya vilabu vingi vya Tanzania kusajili wachezaji wengi ambao wamekuwa hawana msaada kwa timu hizo, kwani wamekuwa wakikaa benchi mda mrefu hivyo kupokea pesa za mishahara bila kazi yoyote.

Rage amefika mbali zaidi na kutolea mfano wa baadhi ya wachezaji wa kigeni ambao walisajiliwa kwa pesa kubwa na wameshindwa kuonesha thamani zao uwanjani hasa wabrazili wa Simba na baadhi ya wachezaji waliosajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu huu kama Issa Bigirimana, Maybin Kalengo na Sadney.

Mbali na hayo kiongozi huyo wa zamani chama cha soka nchini FAT kwa sasa Shirikisho la soka TFF, amependekeza kuwa kama inawezekana ni bora vilabu visajili wachezaji hata 7 ambao watakuwa na uwezo mubwa na wakavisaidia vilabu vyao na sio kuja Tanzania na kupiga pesa.

Gari latumbukia baharini laua watumishi watatu wa Bandari
Vazi la kujikinga na Corona la Muhimbili kuokoa mamilioni ya fedha