Mshambuliaji kutoka nchini England, Raheem Sterling amesema alikua sahihi kuihama klabu ya Liverpool mwanzoni mwa msimu huu na kujiunga na klabu ya Man City.

Sterling, ambaye aliacha gumzo kubwa wakati akifanya maamuzi ya kuondoka kwenye klabu ya Liverpool, amezungumza suala hilo kwa mara ya kwanza kupitia vyombo vya habari ambavyo mara kadhaa vilihitaji kusikia kutoka kwake anazungumziaje juu ya maamuzi aliyoyafanya.

Akiwa katika kambi ya timu ya taifa ya England kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hispania utakaochezwa kesho, Sterling amesema haoni cha kujutia kuchukua maamuzi ya kuachana na Liverpool zaidi ya kujipongeza kwa hatua kubwa aliyopiga.

Amesema anajua mashabiki wengi waliamini huenda alikua amefanya makossa kwa kuihama klabu hiyo ya Anfield, lakini alitambua nini alichokifanya baada ya kupokea ushauri kutoka kwa watu wake wa karibu ambao siku zote wamekua wakimuongoza kwenye maisha yake ya soka.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ameongeza kwamba maisha ya Etihad Stadium anayafurahia, na amekua akiona tofauti kubwa ya uchezaji kwenye kiksoi cha klabu ya Man City ambacho kipo chini ya meneja kutoka nchini Chile Manuel Pellegrini.

Raheem Sterling aliondoka Liverpool, kwa ada ya uhamisho wa pauni million 44 na mpaka sasa ameshaitumikia Man City katika michezo kumi na kufunga mabao manne.

Mpambe wa Karibu Wa Lowassa Akutwa na Hili Mikononi Mwa Polisi
Cesc Fabregas Ajitahidi Kusafisha Hali ya Hewa