Mapigano ya usiku, kati ya makundi yenye silaha yamesababisha vifo vya watu 13 na wengine 30 kujeruhiwa wakiwemo raia katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Mamlaka za Serikali zimesema, mapigano hayo yalizuka katika kitongoji cha Ain Zara, huku kukiwa na hali ya mvutano wa kisiasa unaoongezeka siku baada ya siku.
Mapigano hayo, nadaiwa kuyahusisha makundi mawili yenye silaha yenye nguvu kubwa magharibi mwa nchi hiyo yenye vita kati ya kikosi cha Al-Radaa na Kikosi cha Wanamapinduzi cha Tripoli.
Ingawa, mapigano kati ya makundi yenye silaha ni ya mara kwa mara, hii inakuwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mingi kutokea tukio linalohusisha mauaji ya raia.
Ijumaa, Julai 22, 2022 kundi jingine la Brigade 444, liliingilia kati ili kupatanisha mapatano baina ya makundi hayo lakini na wao pia walianguka katikati ya mapigano mkali na kulazimika kurudi nyuma.
Vyanzo rasmi, vinaonyesha kuwa rais wa Libya, Abdelhamid Dbeibah alimsimamisha kazi waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa nchi hiyo na itikadi za kisiasa zinatajwa kuleta tofauti baina ya makundi hayo hasimu.