Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata raia 17 wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali wakiwa katika gari aina ya Toyota Alphard wakielekea mkoani Mbeya baada ya dereva wa gari hilo kushindwa kusimama katika kizuizi cha polisi Mikumi mkoani humo.
Akizungumza na Dar24Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunas Musilimu amesema gari hilo lilikuwa halina namba za usajili, ambapo gari hilo halikusimama katika kizuizi cha polisi mikumi liliposimimamishwa ndipo akari wakalitilia mashaka gari hilo na kulifuatilia.
“Askari wetu wakastukia kwamba kwanini gari hili majira ya saa kumi na moja alfajiri lipite wakati halina namba za usajilikwaiyo wakaamua walisimamishe walivyolisimamisha yule dereva aliyekuwa anliendesha hilo gari hakusimama akakimbia moja kwa moja akapita kwenye hicho kizuizi kwaiyo askari wakajua moja kwa moja kwamba hili gari lina matatizo kwaiyo wakaanza kulifuatilia”.
Amesema kuwa dereva wa gari hilo aliendesha mpaka eneo la Ruaha Mbuyuni kukaribia kuingia Mkoa wa Iringa ambapo dereva alichepuka barabara kuu na kuingia polini na kulipaki gari akakimbilia kusikojulikana .
“Akatoka nje ya barabara kuu akenda umbali wa km 15 ndani huko porini ndo akalitelekeza lile gari kwaiyo askari wetu walivyofuatilia wakagundua wakafika wakalikuta hilo gari walipoangalia ndani ya gari ndo kukuta hao raia 17 wa ethiopia wakiwa katika hilo gari na dereva alikuwa ametokomea kusikojulikanan,” Amesema Kamanda Musilimu.
Aidha Kamanda Musilimu amesema taratibu za kisheria zimefanyika kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji
Hata hivyo kamanda huyo amesema pia jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa 50 kwa tuhuma mbalimbali katika operesheni ya kupambana na uhalifu iliyoanza Februari 26, 2022.
Kamanda amesema katika operesheni hiyo imewatia nguvuni watuhumiwa 16 wanaojihusisha na kuuza na kusambaza bhangi ambapo viroba vinne vyenye jumla ya kilo 80 huku vijana 13 wakikamatwa kwa kujihusisha na wizi maeneo ya masoko na katika minada ya Kikundi, Sabasaba na soko la Mawenzi.