Raia 29 wa Burundi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam wakikabiliwa na  shtaka moja la kuingia katika Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania bila ya kuwa na vibali maalumu.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Godfrey Gwilo amedai mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa Mei 25 mwaka huu, huko  Kariakoo ndani ya Wilaya  ya Ilala jijini Dar es salaam washtakiwa waliingia nchini kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo washtakiwa 13 walikana kosa hilo na kudai kuwa wana vibali maalumu na wengine 16 walikubaliana na tuhuma hizo na kujibu kuwa ni kweli.

Hakimu amewataka washtakiwa wote walio jitetea si kweli wafike na vibali  vyao (documents) vitakavyoonesha kuwa wana uhalali wa kuishi  nchini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni Mosi mwaka huu na washtakiwa  wote wamerudishwa rumande.

Wizara ya afya kufuatilia wajawazito wote nchini
Dodoma Jiji FC yadai kupuliziwa dawa chumba cha kubadilishia