Watu 29 wameuawa katika mashambulizi ya anga nchini Syria kwenye eneo linalodhibitiwa na waasi karibu na Damascus.
Mauaji hayo yamefanyika wakati vita vya maneno kuhusu matumizi ya gesi ya chlorine dhidi ya raia yakiendelea kushika kasi.
Aidha, mashambulizi hayo yametokea baada ya ufyatuaji wa makombora katika eneo la Ghouta Mashariki, wakati ambapo mzozo wa Syria uliodumu kwa miaka saba ukiwaacha raia wakiteseka.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shirika linaloshughulikia masuala ya haki za binaadamu nchini, Rami Abdel Rahman amesema raia 29 waliuawa na wengine kadhaa walijeruhiwa, ambapo mashambulizi hayo yametokea katika soko kwenye mji wa Beit.
Hata hivyo, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley ameikosoa Urusi kwa kumlinda Rais wa Syria Bashar al-Assad kutowajibishwa kwa kile alichokifanya.