Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imewahukumu raia wawili wa Kichina, Xia Yanan (26) na Chinese Xia Yanan (26) na Mtanzania mmoja, Mtala Habibu, kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya milioni 9.3 za kitanzania kwa kukiuka sheria ya baraza la Mazingira (NEMC).
Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shaidi aliwatia hatiani washtakiwa hao ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya Kichina Jiangxi International (T) Limited, baada ya kukiri kutenda makosa mawili waliyokuwa wakituhumiwa.
Mashtaka hayo ni kushindwa kuchukua tathmini ya uharibifu wa mazingira na kudharau amri halali ,ambapo washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Januari na Agosti 28, 2018 maeneo ya Regent Estate Wilaya ya Kinondoni.
Awali mawakili wa Serikali walidai raia hao kuwa Wamarekani ndio walioanzisha mradi uliokuwa kwenye kitalu no. 306, Regent Estate, ambapo waliendesha ujenzi bila kuzingatia tathmini ya mazingira hivyo waliomba mahakama itoe adhabu ambayo itakuwa fundisho kwao na kwa wawekezaji wengine ambao wanatakiwa kujua Tanzania ina sheria zake.
-
JPM atuma ujumbe mzito Israel
-
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 9, 2018
-
JPM amtumbua balozi wa Tanzania nchini Canada
Hata hivyo, kwa upande wa wakili wa kujitegemea wa washtakiwa hao aliomba Mahakama kutoa adhabu ndogo kwani ni kosa lao la kwanza na wamekubali makosa ili kuokoa muda wa mahakama na gharama nyingine.