Kiongozi mkuu wa ngome ya upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa hatashiriki katika mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2022, badala yake atajikita katika kazi mpya aliyopewa na Tume ya Umoja wa Afrika.
Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu na msemaji wake, Dennis Onyango, mwanasiasa huyo amesema kuwa atajikita katika kujenga miundombinu katika bara la Afrika pamoja na kuwaunganisha Wakenya.
“Bw. Odinga anapenda kuwataarifu kuwa hatajihusisha na siasa za kurithishana madaraka kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022,” taarifa hiyo inasomeka.
“Odinga anataka kutumia miaka kadhaa ijayo kujikita katika kujenga miundombinu barani Afrika kupitia ofisi yake mpya pamoja na kuhakikisha anajenga daraja la kuwaunganisha Wakenya, kupitia kampeni ya ‘Kujenga Daraja Kuelekea Taifa Jipya la Kenya (BBI)’,” ameongeza.
-
Ali Kiba ajibu mualiko wa Diamond Wasafi Festival, ‘kisanii’
-
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 6, 2018
Tangu alipoteuliwa kuwa mwakilishi wa Tume ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya kushughulikia maendeleo ya miundombinu barani Afrika, viongozi mbalimbali wa siasa wamekuwa wakimshauri kuachana na siasa za Kenya na kujikita katika kazi yake hiyo mpya.