Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ambaye ni rafiki wa Dkt. John Magufuli ameeleza jinsi ambavyo chama chake cha ODM na Kenya walivyoupokea ushindi wa kada huyo wa CCM kugombea kiti cha urais wa Tanzania.

Akiongea na kituo cha runinga cha ‘Azam Two’, Odinga alisema kuwa wameufurahia sana ushindi wa Magufuli. Alisema wana imani kubwa kuwa kwa utendaji wake atasaidia kuimarisha zaidi umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Sisi kama rafiki wa Tanzania tumefurahishwa sana na ambayo yamefanyika. Kuteuliwa kwa bwana maguguli kama yule ambaye atabeba bendera ya chama cha CCM, imetufurahisha sana hapa Kenya. Ndio maana sisi tunasema pongezi na heko kwa bwana Magufuli,”alisema Raila Odinga.

Odinga alieleza kuwa amemfahamu Dkt. Magufuli kwa kipindi kirefu na wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na kushauriana tangu walipokuwa wanafanya kazi kama mawaziri wa wizara za ujenzi na barabara wa nchi zao. Hivyo, anatambua uwezo wake wa kutenda kazi kwa ufanisi.

Akielezea jinsi alivyomfahamu Magufuli na kama aliwahi kumdokezea kuwa na mpango wa kuwa rais wa Tanzania siku za usoni, Odinga alisema, “ni mtu mpole, si mtu ambaye ana hamaki. Anafuatilia mambo kabla hajafanya. Yeye mwenyewe amesema tu mara kwa mara eti hawezi kujilazimisha katika hili, lakini watanzania wakiamua yeye atakuwa tayari kuwahudumia hata katika cheo cha urais.”

Alisema chama cha ODM ni rafiki wa Chama Cha Mapinduzi hivyo watakiunga mkono katika mbio hizo za urais wa Tanzania japo hawatajihusisha moja kwa moja na kampeni kwa kuwa kampeni zinapaswa kufanywa na watanzania wenyewe.

Mkanda Wa Ngono Wa Mama Mtoto Wa Rick Ross Wamfilisi 50 Cent
Rais Atoa Tamko Juu Ya Tajiri wa ‘Unga’ Aliyetoroka Jela Yenye Ulinzi Mkali