Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua ameonesha kuwa na mashaka na urafiki wa Kiongozi wa azimio la Umoja Raila Odinga na Mwanasiasa George Wajackoya ambaye amekuwa akihamasisha matumizi ya Bangi akisema hauwezi kuleta faida bali matatizo katika jamii.

Gachakua ameyasema hayo wakati akiongelea juu ya kile kilichotukia hapo jana Julai 12, 2023 baada ya Maandamano ya kupinga ukali wa maisha kuacha simanzi kufuatia ripoti ya vifo vya Watu sita vilivyotokea katika miji ya Mlolongo na Kitengela nje kidogo ya mji mkuu wa Nairobi.

Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.

Amesema, “mimi nilifikiria hawa watu wa Azimio walisoma wako na akili ya kuweka sufuria kwa kichwa, lakini nilipoona wanatembea na Wajackoyah nikajua hawa watu hawana akili. Mnatembeaje na mtu wa Bangi? hivi ”Raila unataka kuua watu wangapi ndio utosheke? Hiyo damu unataka kuenda kufanyia nini?.

Aidha, DP Gachagua ameongeza kuwa “sisi tuko na askari na Bunduki, nyinyi mko na pesa. Sasa ni nyinyi kuamua juu bunduki ziko na risasi, penyewe tumefika saa hii ni sawa tu, wacha tuone vile itakuwa tumechoka na hawa watu.”

PSG kumng'oa Victor Osimhen SSC Napoli
Aubameyang kuvutwa Saudi Arabia