Rais wa Lebanon, Michel Aoun (89), ambaye ameiongoza nchi hiyo inayokabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na mlipuko mbaya wa bandari ya Beirut, anaondoka madarakani hii leo (Oktoba 30, 2022) huku akiacha ombwe la utawala.
Bunge la nchi hiyo, hadi sasa halijaweza kuafikiana ili kumpata mrithi wa Aoun, ambaye nusu ya muda wake wa uongozi, alitawala na baraza la muda la Mawaziri.
Baadhi ya wafuasi walikusanyika ikulu ya baada kumuaga kiongozi huyo ambaye alipata urais mwaka 2016 katika makubaliano ambayo yalimleta mwanasiasa mkuu wa wakati huo, Saad al-Hariri, kurejea madarakani kama Waziri Mkuu.
Hata hivyo, hatua yake ya mwisho kiutendaji akiwa kama rais wa nchi hiyo, ilikuwa ni utiaji saini makubaliano na taifa la Israel, kuhusu mpaka wao wa bahari ya kusini, mkataba ambao ulifikiwa baada ya upatanishi wa Serikali ya Marekani.