Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Waziri Waziri kundamba kuwa Mkuregenzi Mkuu wa shirika hilo.
Amefanya uteuzi huo leo na amewataka wakurugenzi hao kuchapa kazi kwa juhudi na kuhakikisha TTCL inaongeza ufanisi na kutoa gawio kwa serikali.
Kabla ya uteuzi huu Dkt.Omari Rashid Nundu alikuwa Mwenyeki wa Bodi ilikyokuwa kampuni ya Simu Tanzania, Tanzania Telecommunication Company Limited (TTCL). Na Waziri Waziri Kindamba alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo.
Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwahamisha wafanaykazi wote na maafisa wa Umma wa iliyokuwa TTCL kwenda TTCL Corparation.
Pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kutoivunja bodi hiyo na kutaka wajumbe wote kuendelea na nafasi zao na kujaza nafasi za wajumbe zilizobaki.
Uteuzi huo umefanyika mara baada ya Rais kupokea taarifa kutoka kwa viongozi wa Shirika hilo la simu Tanzania kuhusu mwelekeo wa Shirika baada ya kuanza kutumika kwa sheria namba 12 ya mwaka 2017 ya shirika la Simu Tanzania iliyolibadili kutoka kampuni ya simu Tanzania TTCL na kuwa Shirika la simu Tanzania TTCL tangu 01, Februari 2018.
Dkt. Omari Rashid Nundu na Waziri Waziri Kindamba wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uteuzi huo na wamesema TTCL itaendelea kujiimarisha kwa kupanua huduma za mawasiliano nchini, kuongeza na kuboresha bidhaa ikiwemo TTCL pesa, kuzalisha faida na kuusimamia vizuri mkongo wa Taifa kwa maslahi na usalama wa nchi.