Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameipiga simu kwa familia ya Waziri wa Nchi, Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda, Kanali Mstaafu Charles Okello Engola, ili kuwafariji baada ya kupigwa risasi na mlinzi wake nyumbani kwake eneo la Kyanja, lililopo jijini Kampala.

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari na ICT, Chris Baryomunsi amesema Rais Museveni alitaka kujua mazingira ambayo waziri huyo aliuawa wakati alipokuwa akielekea kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kabla ya kushambuliwa kwa risasi.

Kutoka kushoto: Waziri wa Usalama wa Uganda, Jim Muhwezi, Naibu Spika, Tayebwa na Waziri wa Nyumba, Sam Engola, wengine ni watumishi wa vyombo vya usalama wakiendelea na taratibu baada ya tukio hilo loa mauaji. Picha na The Kampala Report.

Engola aliuawa na mlinzi wake, askari wa UPDF, ambaye Naye alijiuwa kwa risasi akidai Waziri huyo alikuwa akimtendea vibaya ambapo pia Naibu Spika wa Bunge, Thomas Tayebwa akiwa ni miongoni mwa Viongozi Serikali waliotembelea nyumbani kwa waziri huyo muda mfupi baada ya kuuawa.

Naye Mshauri Mkuu wa Rais kuhusu operesheni maalum Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aliandika katika ukurasa wake wa twitter, “Inasikitisha sana kusikia kuhusu kifo cha kusikitisha cha Kanali (mst) Charles Engola, ni hasara ya kutisha kwa nchi. Roho yake ipumzike kwa amani ya milele.”

Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Thomas Tayebwa akiwa na familia ya Waziri Engola nyumbani kwao Kyanja. Picha ya The Kampala Report.

Kwa upande wake Kiongozi wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa wa Upinzani, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine), alisema “Uganda hakuna aliye salama. Hata wale wanaoidumisha. Pumzika kwa amani Kanali Mstaafu Charles Okello Engola. Pole kwa familia na wananchi wa Kitongoji cha Lango.”

Kocha Marumo Gallants kuitumia Simba SC Dar
Michael Owen aishauri Liverpool usajali 2023/24