Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, Joseph Kabila, amekanusha shutuma za nchi jirani ya Uganda, kwamba alitoa hifadhi kwa kundi la waasi wa Kiislamu, na kuliruhusu kutumia rasilimali za madini.

Hatua hiyo imekuja kufuatia madai ya wiki iliyopita, ambapo Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kusema Kabila aliruhusu wanamgambo wa Allied Democratic Forces – ADF, kundi lenye uhusiano na Magaidi wa Islamic State – IS, kujenga kambi kubwa, kuchimba dhahabu na kuuza mbao.

Kabila amesema, “Madai ya uongo ya Rais Museveni, ambaye ni mmoja wa wahalifu wakuu katika eneo hilo, hiyo ni kejeli tu, na madai yake pia yanalenga kuwavuruga watu wa Kongo na kuwagawanya kamwe sitakubali na anapaswa kupuuzwa.”

Kundi la ADF, ambalo lilianzishwa mwaka 1996, awali ilikuwa kundi la waasi wa Uganda, wakifanya mashambulizi katika eneo la Rwenzori magharibi mwa nchi hiyo na walifukuzwa eneo hilo huku waliobakiia, wakivuka mpaka na kuingia misitu ya mashariki mwa Kongo kujihifadhi.

Dusan Vlahovic aingia anga za PSG
Harry Maguire kuibukia Chelsea?