Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo amesherehekea kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kundi lake la kisiasa la African People’s Party – Côte d’Ivoire jijini Abidjan.

Wakati wa mkutano wa kuadhimisha hafla hiyo, mzee huyo mwenye umri wa miaka 77, alitoa maoni ya kwanza rasmi kuhusu kuzuiliwa kwa wanajeshi 46 wa Ivory Coast nchini Mali, ambao walikamatwa walipofika Bamako Julai 10, 2022 na walishtakiwa kuwa mamluki.

Gbagbo amesema, “Rais Assimi Goïta (mkuu wa junta ya Mali), anapaswa kuulizwa kufikiria juu ya udugu wake wa silaha na wale (askari wa Ivory Coast) ambao wako gerezani huko.”

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo na mkewe Simone Gbagbo baada ya kukamatwa Hotelini na vyombo vya usalama nchini humo kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo kuhusika na vurugu wakati wa uchaguzi mwaka 2022 . Picha: BBC

Kiongozi wa chama cha PPA-CI alitoa wito kwa rais wa Togo, ambaye ndiye mpatanishi wa mgogoro huo kuzidisha juhudi zake kusaidia kutatua mzozo huo wa kidiplomasia.

Wakati wa mkutano huo, mada zilielekezwa kwenye siasa za ndani na kinyang’anyiro cha urais wa 2025, na ikiwa Gbagbo hajatangaza rasmi zabuni yake, kwa katibu mkuu ni ukweli ulio wazi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025, Gbagbo akiwa mgombea wa asili.

Rais wa sasa wa Ivory Coasty, Alassane Ouattara ameiongoza nchi hiyo tangu 2010 ambapo mbali na chama cha Gbagbo, vyama vingine vya upinzani vya nchi hiyo ni pamoja na (PDCI), cha kiongozi wa zamani Henri Konan Bédié, na (MGC) cha Simone Gbagbo, ambaye ni mke wa rais huyo wa zamani, Laurent Gbagbo.

Zahera atuma ujumbe Young Africans akiitumia SImba SC
Mwinyi Zahera: Ibrahim Ajibu bado wamo