Rais wa Liberia George Weah amemfuta kazi Waziri wa Sheria, Charles Gibson na kumteua Musa Dean aliyekuwa wakili katika Tume ya Uchaguzi kushika nafasi hiyo.
Rais Weah amechukua uamuzi huo baada ya malalamiko kutoka kwa wateja ambao amekuwa akiwasimamia kesi zao kulalamika kuwa wakili huyo anawatapeli.
Kufuatia utenguzi huo wakili Gibson tayari amekwisha pokonywa leseni yake ya uwakili.
Kabla ya uteuzi wake Gibson alipatikana na hatia na Mahakama ya juu baada ya kumtapeli mteja wake dola za Marekani 25,00. Mahakama hiyo alimwamuru kuzirejesha fedha hizo.
Mwanasoka huyo wa zamani wa Liberia ambaye sasa ni Rais, George Weah aliteuliwa nafasi hiyo, Januari, 22 mwaka huu akiwa katika jaribio lake la pili toka awanie urais wa nchi hiyo.